Matthew 14:1-6

Yahya Mbatizaji Akatwa Kichwa

(Marko 6:14-29; Luka 9:7-9)

1 aWakati huo, Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za Isa, 2 bakawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yahya Mbatizaji; amefufuka kutoka kwa wafu! Hii ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

3 cHerode alikuwa amemkamata Yahya, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, 4 dkwa kuwa Yahya alikuwa amemwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.” 5 eHerode alitaka sana kumuua Yahya, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii.

6Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria, akamfurahisha sana Herode,
Copyright information for SwhKC